Pata taarifa kuu
COLOMBIA

UN kutuma wajumbe wake kuwasaidia waasi wa zamani wa FARC kurejea kwenye jamii

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limeamua kutuma ujumbe nchini Colombia kwenda kuwasaidia wapiganaji wa zamani wa FARC kurejeshwa na kupokelewa kwenye jamii.

Waasi wa zamani wa FARC nchini Colombia
Waasi wa zamani wa FARC nchini Colombia LUIS ROBAYO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ngumu inakuja baada ya waasi hao kukubali kuweka silaha chini na kumaliza zaidi ya miaka 50 ya mapigano kati yao na wanajeshi wa serikali.

Wakati uo huo, rais Juan Manuel Santos amewapa msamaha waasi hao wa zamani wapatao 3,600 na kufikia idadi ya waasi waliosamehewa kufikia 7,000.

Mapigano hayo ya zaidi ya miaka 50 yalisababisha vifo vya watu 260,000.

Hata hivyo, watu zaidi ya 60,000 hawajulikani waliko huku wengine Milioni saba wakiyakimbia makwao kutokana na mzozo huu ambao umedumu kwa muda mrefu duniani.

Mkataba wa kumaliza mapigano kati ya pande zote mbili, ulifikiwa mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.