Pata taarifa kuu
MAREKANI-VATICAN-USHIRIKIANO

Donald Trump kukutana na Papa Francis

Donald Trump aliwasili Jumanne jioni May 23 katika mji wa Roma, ziara yake ya kwanza barani Ulaya tangu kucukua hatamu ya uongozi wa Marekani. rais Donald Trump atakutana Jumatano hii asubuhi na kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, katika mji wa Vatican.

Le couple présidentiel américain s'embarque à bord d'Air Force One pour se rendre à Rome-Fiumicino, le 23 mai 2017.
Le couple présidentiel américain s'embarque à bord d'Air Force One pour se rendre à Rome-Fiumicino, le 23 mai 2017. REUTERS/Jonathan
Matangazo ya kibiashara

Ndege ya rais wa Marekani, Air Force One, ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Fiumicino mjini Roma siku ya Jumanne Mei 23 saa 12 jioni, ambapo hatua muhimu za usalama ziliwekwa. Rais wa Marekani anakutana na Papa Francis Jumatano hii Mei 24 asubuhi katika mji wa Vatican. Mazungumzo yao yatagubikwa hasa na vikwazo dhidi ya wahamiaji, kushirikiana kiuchumi, mauzo ya silaha, adhabu ya kifo na mengineyo. Wawili hao pia huenda wakazungumzia kuhusu mapambano dhidi ya utoaji mimba.

Baada ya mkutano huo, rais Donald Trump na mkewe wanazurumaeneo matakatifu kwa Wakatolika ya Sistine Chapel na kanisa kuu la Mtakatifu Petro. Baada ya kuzuru maeneo hayo, rais Donald Trump atakutana na rais pamoja na Waziri Mkuu wa Italia katika Ikulu ya Quirinal, wakati ambapo mke wake Melania atatembelea watoto wagonjwa katika hospitali ya Bambino Gesù na binti yake ambaye ni mshauri wa babke, Ivanka atatembelea jamii ya Wakatoliki wa dhehebu la Sant 'Egidio, katikati mwa mji wa Roma, kujadili mapambano dhidi ya biashara yaya wahamiaji.

Hii ni hatua ya tatu ya ziara ambayo tayari imemfikisha Donald Trump nchini Saudi Arabia, Israeli na Palestina na itaendelea hadi Brussels katika mkutano wa umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi (NATO) na katika mji wa Sicily ambako atahudhuria mkutano wa chi saba zenye nguvu duniani (G7).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.