Pata taarifa kuu
NASA-DUNIA-MWEZI

Jiwe kubwa lapita salama karibu na Dunia

Jiwe kubwa maarufu kama Asteroidi ambalo inakadiriwa kuwa na kipenyo cha karibu kilomita moja, iilipita salama karibu na dunia umbali wa mara tano hivi, umbali kati ya Dunia na Mwezi.

Jiwe kubwa ambalo linakadiriwa kuwa na ukubwa karibu sawa na wa Jiwe la Gibraltar (kwenye picha) limepita salama karibu an Dunia.
Jiwe kubwa ambalo linakadiriwa kuwa na ukubwa karibu sawa na wa Jiwe la Gibraltar (kwenye picha) limepita salama karibu an Dunia. AFP PHOTO / CNRS / F. d'Errico
Matangazo ya kibiashara

Inaaminika kwamba Asteroidi hiyo inakadiriwa kuwa na ukubwa sawa na Jiwe la Gibraltar.

Wataalamu wa maswala ya anga wamesema Jiwe hilo ambalo limepewa jina la 2014 JO25, ndilo kubwa zaidi kupita karibu na dunia tangu 2004. Hata hivyo wamebaini kwamba fursa nzuri zaidi ya kutazama asteroidi hiyo angani ilitokea siku ya Jumatano usiku.

Kwa mujibu wa Shirika la Anga la Marekani (Nasa) picha zilizopgwa zinaonesha kwamba jiwe hilo lenye umbo la njugu linazunguka mara moja kila baada ya saa tano.

Inakadiriwa kwamba jiwe jingine kupita karibu na dunia itakuwa mwaka 2027. Inaarifiwa kwamba asteroidi ya kipenyo cha karibu mita 800 iliyopewa jina 1999 AN10 itapita karibu na dunia umbali sawa na wa mwezi kutoka kwa Dunia, takriban 380,000 km.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.