Pata taarifa kuu
COLOMBIA

Maporomoko ya ardhi nchini Colombia yasababisha vifo vya zaidi ya watu 200

Maporomoko ya ardhi mjini Mocoa nchini Colombia yamesababisha vifo vya 254 wakiwemo watoto 43.

Hali ya maporomoko ya ardhi nchini Colombia
Hali ya maporomoko ya ardhi nchini Colombia wordpress.com
Matangazo ya kibiashara

Rais Juan Manuel Santos amesema nchi yake inaomboleza kutokana na mauaji hayo makubwa yaliyosababisha na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Rais Santos, alizuru mji huo ulipo Kusini mwa nchi hiyo kujionea mwenye hali ilivyokuwa, na kuonya kuwa huenda idadi ikaongezeka.

“Tunawaombea wale wote waliothirika.Tunatuma risala zetu za rambirambi kwa wananchi wote wa familia zilizoathirika.”

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis naye ametuma risala za rambirambi na kusema kuwa anawaombea wananchi wa Colombia.

Mbali na vifo hivyo, maporomoko hayo yamesababisha watu wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa na kusababisha uharibifu wa mali.

Waokozi na watalaam wengine wanaendelea na juhudi za kuwatafuta watu ambao bado hawajafahamu walipo.

Mbali na Colombia, mataifa mengine ya America Kusini ambayo yameathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha ni pamoja na Peru na Ecuador.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.