rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Colombia FARC

Imechapishwa • Imehaririwa

Colombia kuanzisha mfumo maalum wa mahakama kushtaki uhalifu wa kivita

media
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos (kushoto) na kiongozi mkuu wa FARC Timoleon Jimenez (kulia), pamoja na Rais wa Cuba Raul Castro, Juni 23, 2016 mjini Havana. REUTERS/Alexandre Meneghini

Mfumo wa mahakama ni jambo muhimu kwa mkataba wa amani kati kundi la waasi la FARC na serikali ya Juan Manuel Santos. Nakala tayari imepitishwa na wabunge.


Mageuzi yanaazisha "mfumo muhimu vyombo vya sheria, ukweli, fidia na kutorudia kosa", ambao ni pamoja na mambo matatu: Tume ya Ukweli, kitengo kwa ajili ya kutafuta watu waliotoweka wakati wa mgogoro kati kundi la waasi la FARC na vikosi vya serikali, na mahakama maalum kwa ajili ya amani (JEP).

Mwaka jana serikali ya Colombia na kundi la waasi la FARC walitiliana saini mkataba wa amani wa kumaliza mapigano yaliyodumu kwa miongo mitano nchini humo.
Mkataba huo wa kihistoria ulitiwa saini na Rais wa Colombia Juan Manuel Santos na kiongozi wa waasi wa FARC Timoleon Jimenez.

Zaidi ya watu 2500 wakiwepo watu mashuhuri walihudhuria hafla hiyo akiwemo rais wa CUBA, Raul Castro ambaye alikuwa msuluhishi wa mgogoro huo kwa kipindi cha miaka minne tangu mwaka 2012.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Colombia vilidumu miaka 42 ambapo maelfu ya watu walipoteza maisha.