Pata taarifa kuu
CANADA-UISLAM-MAUAJI

Mtuhumiwa mmoja wa mauaji ya Quebec akamatwa

Polisi ya jimbo la Quebec nchini Canada inasem akuwa inamchukulia mmoja wa watu wawili waliokamatwa kama mtuhumiwa wamauaji ya watu sita waliouawa kwa kupigwa risasi katika Msikiti mjini Quebec.

Maafisa wa polisi wakitembea karibu na Msikiti ambapo kulizuka ufyatulianaji risasi katika mji wa Quebec, mkoa unaozungumza Kifaransa magharibi mwa Canada, tarehe 29 Januari.
Maafisa wa polisi wakitembea karibu na Msikiti ambapo kulizuka ufyatulianaji risasi katika mji wa Quebec, mkoa unaozungumza Kifaransa magharibi mwa Canada, tarehe 29 Januari. REUTERS/Mathieu Belanger
Matangazo ya kibiashara

Jumapili usiku watu sita waliokuwa wamejihami kwa silaha walivamia msikiti mmoja mjini Quebec nchini Canada, na kusababisha vifo vya watu sita na wengine wanane kujeruhiwa.

Waziri Mkuu Justin Trudeau ameshtumu shambulizi hili na kuliita kuwa la kigaidi.

Polisi inasema tayari imewakamata watu wawili wanaohusishwa na shambulizi hilo. Mji wa Quebec ni makaazi ya watu wengi wanaozungumza lugha ya Kifaransa.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande, naye amelaani shambulizi hili na kusema magaidi hao walijaribu hali ya amani ya mji huo.

Aidha, amesema kuwa serikali yake na Canada zitaendelea kushirikiana ili kushinda ugaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.