Pata taarifa kuu
CUBA-CASTRO

Mwanamapinduzi wa Cuba Fidel Castro azikwa

Baada ya siku tisa za maombolezo ya kitaifa, majivu ya Fidel Castro yamefikia hatua ya mwisho. Rais wa zamani wa Cuba amezikwa Jumapili hii, Desemba 4, 2016 katika makaburi ya St Iphigenia mjini Santiago de Cuba.

Umati wa watu ukikuja kutoa heshima zamwisho kwa Fidel Castro, Desemba 3, 2016 katika mji wa Santiago de Cuba, ambapoalizikwa mwanamapinduzi wa mwaka 1959.
Umati wa watu ukikuja kutoa heshima zamwisho kwa Fidel Castro, Desemba 3, 2016 katika mji wa Santiago de Cuba, ambapoalizikwa mwanamapinduzi wa mwaka 1959. JUAN BARRETO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumapili hii nchini Cuba, iliku mwisho wa siku tisa ya kutoa heshima za mwisho kwa Fidel Castro, aliyefariki Novemba 25 akiwa na umri wa miaka 90. Majivu ya mwili wa Fidel Castro yalisafirishwa nchini kote kwa muda wa siku hizi tisa za maombolezo ya kitaifa chini ya ulinzi mkali, huku majivu hayo yakiwekwa katika sanduku dogo lililokua likibebwa na gari dogo aina ya jeep.

Santiago de Cuba ni mji ambapo vita vya maguguni vilianza. Mwanamapinduzi huyo wa Cuba amezikwa katika eneo alikozikwa mwasisi wa uhuru wa kisiwa hicho José Martí.

Wacuba walimiminika kwa wingi kwa kuja kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanamapinduzi kama ilivyokua katika miaka ya 1959, wakati Fidel Castro alipata ushindi wa vita vya maguguni na kuingia katika mji wa Havana baada ya kuanguka kwa utawaa wa Fulgencio Batista. Santiago de Cuba ni mji mkuu wa mashariki mwaCuba, moja ya miji ya kale ya kisiwa hicho na "eneo" kulikoanzia mapinduzi.

Fidel Castro, ambaye hakutaka kuzikwa karibu na familia yake amezikwa eneo alikozikwa mshairi na mwanasiasa wa Cuba José Martí, mwanzilishi wa Chama cha Mapinduzi nchini Cuba katika mwaka 1892. Lakini pia amezikwa katika eneo walikozikwa askari wenzake Julai 26, 1953, waliouawa katika shambulio la kwanza lililoshindwa katika kambi ya kijeshi ya Moncada.

Makaburi ya eneo la St Iphigenia mjini Santiago de Cuba, yalipigwa picha kwa umbali wakati wa mazishi ya Fidel Castro siku ya Jumapili tarehe 4 Desemba.
Makaburi ya eneo la St Iphigenia mjini Santiago de Cuba, yalipigwa picha kwa umbali wakati wa mazishi ya Fidel Castro siku ya Jumapili tarehe 4 Desemba. YAMIL LAGE / AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.