Pata taarifa kuu

Kifo cha Fidel Castro: wiki ya maadhimisho kuanza nchini Cuba

Raia wa Cuba wanaendelea kuomboleza kifo cha kiongozi wao wa zamani na Mwanamapinduzi Fidel Castro aliyefariki dunia mwishoni Mapema asubuhi Jumamosi Novemba 26, 2016.

Mji wa Havana, Novemba 27, 2016, unajiandalia mfululizo wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Fidel Castro.
Mji wa Havana, Novemba 27, 2016, unajiandalia mfululizo wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Fidel Castro. REUTERS/Enrique de la Osa
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Jumatatu hii Novemba 28 kwa wiki nzima, Wacuba wataweza kuhudhuria au kushiriki katika mfululizo wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Fidel Castro.

Sherehe mbalimbali zimeanza Jumatatu hii, Novemba 28, siku tatu baada ya kifo cha Fidel Castro. Wacuba wameanza kukusanyika karibu na eneo la kihistoria katikati mwa mji mkuu wa Cuba, ambapo ni eneo la mapinduzi. kundi dogo kutoka Biran, kijiji alikozaliwa Fidel Castro, wamekuja hasa kwa ajili ya tukio hilo.

Saa 2:00 asubuhi saa za Cuba (sawa na saa 7:00 saa za kimataifa), Rais Raul Castro atalihutubia taifa chini ya sanamu la Jose Marti, kiongozi mashuhuri kwa uhuru wa Cuba katika karne ya kumi na tisa mwasisi wa mapinduzi, itikadi alizorithi Fidel Castro. Kisha saa 3:00 asubuhi saa za Cuba, mizinga itapigwa kwa wakati mmoja katika miji ya Havana na Santiago.

Maeneo yote ya burudani yalifungwa huku michezo mbalimbali ikisitishwa, na wanafunzi wa vyuo vikuu jijini Havana waliwasha mishumaa kama ishara ya kumbukumbuka kiongozi wao wa zamani.

Viongozi mbalimbali wa dunia wamekuwa wakitoa risala za rambirambi kwa watu wa Cuba kwa kumpoteza kiongozi ambaye wamemleza kama mtu aliyeibadilisha nchi yake.

Hata hivyoBaadhi ya raia wa Cuba waliokimbilia nchini Marekani wakati wa uongozi wa Fidel Castro walisherehekea kifo chake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.