Pata taarifa kuu
COLOMBIA-SANTOS

Santos atangaza kuwapa fedha za tuzo ya Nobel kwa wahanga wa machafuko

Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos, ametangaza kuwa atawapa fedha za tuzo ya amani ya Nobel aliyotunukiwa hivi karibuni wahanga wa machafuko yaliyoikumba nchi ya Colombia kwa kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja.

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel.
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel. IVAN VALENCIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Juan Manuel Santos alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel Oktoba 7, kutokana na mchango wake katika mazungumzo ya amani aliyoanzisha na kundi la waasi la FARC.
Juan Manuel Santos anaona tuzo hili kuwa ni motisha kubwa na amerudi kusema kuwa anachangia tuzo hiyo na wananchi wa Colombia.

Kutunukiwa tuzo kwa rais Juan manuel Santos kumeibua upinzani mkali miongoni mwa baadhi ya wananchi wa Colombia ikiwa ni pamoja na kiongozi wa kundi hilo na rais wa zamani wa Colombia Alvaro Uribe, aliyeongoza kampeni za kuhimiza wananchi wa Colombia kutopigia kura mazungumzo yaliyofikiwa na kundi la waasi wa FARC.

Katika kura ya mano iliyopigwa Oktoba 3, wapiga kura walikataa kwa idadi ndogo ya wengi makubaliano yaliyosainiwa na kundi la FARC. Kulingana na matokeo rasmi, kura ya maoni ya 'Hapana' ilishinda kwa 50.21% dhidi ya kura ya 'Ndiyo' ambayo ilipata 49.78%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.