Pata taarifa kuu
MAREKANI-UGAIDI

Obama kuhutubia katika kumbukumbu ya Miaka 15 tangu shambulizi la Septemba 11,2001

Marekani inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kutekelezwa kwa shambulizi la kigaidi septemba 11 hii leo kuwakumbuka waathirika wa shambulizi hilo katika ardhi ya Marekani ambalo linaripotiwa kubadili ulimwengu.

Jengo la kimataifa la bishara WTC likiungua baada ya kushambuliwa september 11 2001
Jengo la kimataifa la bishara WTC likiungua baada ya kushambuliwa september 11 2001 DR
Matangazo ya kibiashara

Takribani watu elfu tatu waliuawa September 11, 2001 wakati washambuliaji wa kujitoa muhanga wapatao kumi na tisa waliposhambulia maghorofa jijini New York na Penthagon huko washington na Pennsylvania.

Lilikuwa shambulizi la kwanza kutoka nje ya Marekani katika kipindi cha karne mbili na kusababisha Marekani kuongoza uvamizi wa kijeshi nchini Afghanstan (2001) na Iraq 2003, ambako vita vilirindima kwa zaidi ya muongo baadae.

Hii leo katika maadhimisho hayo majina ya waliopoteza maisha yatasomwa katika ibada ya kumbukumbu jijini New York katika jengo jipya la World Trade Center.

Aidha raisi wa marekani Barack Obama anatarajiwa kuhutubia katika shughuli hizo huko Penthagon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.