Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC

Colombia: FARC na serikali kusaini mkataba wa kihistoria

Nchi ya Colombia inaelekea kupiga hatua katika mchakato wa amani. Kundi la waasi la FARC na serikali ya Colombia wanatazamia kutia saini leo Alhamisi kwenye mkataba kudumu wa usitishwaji mapigano mjini Cuba.

Wapiganaji wa wakundi la waasi wa FRC wakipiga doria katika milima ya jimbo la Cauca, Colombia, Februari 15, 2013.
Wapiganaji wa wakundi la waasi wa FRC wakipiga doria katika milima ya jimbo la Cauca, Colombia, Februari 15, 2013. LUIS ROBAYO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na mkataba huu, nchi inatazamiwa kugeuza ukurasa wa miaka hamsini ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Taarifa hii ilitangazwa Jumatano mchana wiki hii.

Kundi la waasi wa FARC ndio wameanza kukubali kuweka chini silaha na kutia mbele mazungumzo. Mmoja wa maafisa wa jeshi la kundi hilo alianza tokajana kutoka jana kurusha taarifa zake kwenye mitandao ya kijamii ya hashtag "siku ya mwisho ya vita nchini Colombia" (#UltimoDiaDeLaGuerra).

Kisha Ikulu ya rais ikarasimisha taarifa hiyo: Silaha za kivita sasa zitasalia kimya nchini Colombia, kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha nusu karne. Machafuko nchini Colombia yameababisha vifo vya watu wasiopunga 220,000 na mtu mmoja kati ya watu saba alikimbia machafuko hayo.

Alhamisi hii, Rais wa Colombia, Juan Manuel Santos, na wawakilishi wa kundi la waasi la FARC watatia saini kwenye mkataba wa usitishwaji mapigano lakini pia kutangaza jinsi gani waasi kutoka kundi hilo watakusanywa na jinsi watakavyopokonywa silaha chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa. "Tukio hili litaongozwa na rais, kiongozi wa kundi la waasi la FARC Timoleón Jimenez, na wadhamini wa makubaliano hayo: kwa upande wa Cuba, Rais Raul Castro, na Norway, Waziri wa Mambo ya Nje, Borge Brende," amesema Marcela Durán, mwakilishi wa ujumbe wa serikali ya Colombia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon pia anatazamiwa kuhudhuria tukio hilo la kihistoria nchini Cuba.

Katika wiki zijazo, mazungumzo hayo yatafafanua masuala yaliyoachwa kiporo katika kipindi cha miaka mitatu na nusu ya mazungumzo. Pia watafafanua jinsi gani raia wa Colombia watapiga kura juu ya makubaliano hayo. Ofisi ya rais, inataka kura ya maoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.