Pata taarifa kuu
BOLIVIA-KURA YA MAONI-MORALES

Bolivia: kura ya hapana yashinda

Raia wa Bolivia wamekataa katukatu Jumapili hii katika kura ya maoni kumruhusu Rais Evo Morales kugombea muhula wa nne ili kubaki madarakani mpaka mwaka 2025, kulingana na matokeo rasmi yaliotangazwa kwenye televisheni.

Rais wa Bolivia Evo Morales (kushoto), Februari 21, 2016 katika mji wa Villa 14.
Rais wa Bolivia Evo Morales (kushoto), Februari 21, 2016 katika mji wa Villa 14. FP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wapiga kura milioni 6.5 nchini Bolivian walitakiwa kupiga kura Jumapili kwenye marekebisho ya katiba. Na kulingana na matokeo ya awali, kura ya "hapana" inaongoza.

Kura ya maoni imependekeza kurekebisha Katiba ili kumruhusu au la, Rais Evo Morales kuwania muhula wa nne katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2019.

Katika miezi ya hivi karibuni, nchi hii ilikumbwa na hali ya sintofahamu kati ya raia wanaomuunga mkono Rais Evo na wale wanaompinga. Kwa wafuasi wake, kiongozi wa asili ni shujaa wa raia, lakini kwa wapinzani wake, ni dikteta mwenye nguvu ambaye anataka kwa gharama zote kubakia madarakani.

Katika maeneo karibu yoye nchini Bolivia, kura ya hapana imefiki 52%, kwa mujibu wa matokeo ya awali. Matokeo hayani ya muda. Na matokeo ya mwisho ya kura ya maoni yatajulikana ndani ya siku mbili au tatu.

Kura hii ya maoni imekabiliwa na hali tete baada ya vifo vya watu sita wakati wa ofisi za manispa ya jiji iliposhambuliwa na upinzani na huku kukiwa na madai ya rushwa.

Hadi wiki iliyopita, watetezi wa mageuzi ya kikatiba ili kumruhusu rais mkongwe madarakani katika eneo nzima la Amerika ya Kusini kuwania muhula mpya mwaka 2019, katika kipindi cha 2020-202, walikua katika njia moja na
wapinzani.

Lakini tuhuma za kuuza ushawishi zinazomlenga zimeanza kubadili mwelekeo. Katika utafiti wa hivi karibuni, kura ya hapana zilifikia (47%) zikiwa mbele kabisa ya kura za ndio ambazo zilifikia (27%).

Kama hali hii itathibitishwa, itakuwa kushindwa kwake kwa mara ya kwanza tangu kuingia madarakani miaka kumi iliyopita, hata kama chama chake, cha MAS, tayari kimemepoteza katika uchaguzi wa manispaa mwaka 2015.

Bw Morales, mwenye umri wa miaka 56, na Rais wa kwanza wa Bolivie kutoka barani Amerika mwenye asili ya Kihindi, anatuhumiwa kutumia ushawishi wake katika neema ya mpenzi wake wa zamani, Gabriela Zapata. Zapata, mwenye umri wa miaka 28, ambaye ni kiongozi wa kampuni ya Kichina ya CAMC alisaini mikataba na serikali kwa kitita cha Dola milioni 576 (sawa na Euro milioni 516).

Uchunguzi unaendelea

Karibu wiki mbili baada ya kesi hii kuanza, rais alikanusha. "biashara gani ya ushawishi, wote huo ni uzushi uliopangwa na ubalozi wa Marekani," Rais Evo Morales alituhumu. Ili kumchafua katika kura ya maoni,alisisitiza.

Mmoja wa mawaziri wake pia alimshutumu mwandishi wa habari, Carlos Valverde, ambaye alikua mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi mwaka 1990, kwamba ni afisa wa Ubalozi wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.