Pata taarifa kuu
HAITI-UCHAGUZI-MVUTANO-SIASA

Haiti: Jocelerme Privert achaguliwa kuwa rais wa mpito

Jocelerme Privert, mwenye umri wa miaka 62, amechaguliwa na Bunge katika duru ya pili ya uchaguzi kuwa rais wa mpito wa Haiti.

Jocelerme Privert amechaguliwa kuwa rais wa mpito wa Haiti, katika mji wa Port-au-Prince, Februari 14, 2016.
Jocelerme Privert amechaguliwa kuwa rais wa mpito wa Haiti, katika mji wa Port-au-Prince, Februari 14, 2016. REUTERS/Andres Martinez Casares
Matangazo ya kibiashara

Jocelerme Privert amerejelea nafasi ya Michel Martelly ambaye amemaliza muhula wake tarehe 7 Februari bila kukabidhi madaraka kwa mtu mwengine, ambaye angeliendelea kuongoza taifa hilo.

Sababu iliyopelekea uchaguzi huo wa haraka wa rais wa muda ni muda usiojulikana wa kuahirishwa kwa duru ya pili ya uchaguzi wa rais kutokana na pingamizi kutoka vyama vya upinzani.

Pamoja na uchaguzi huu, Haiti imeonekana kuondokana na tishio la kipekee la kutokua na taasisi kwa kipindi kisichojulikana. Katika mkataba uliosainiwa saa chache kabla ya Michel Martelly kumaliza muhula wake, Bunge lilikua lilipewa jukumu la kumchagua kwa siku 120, rais wa mpito.

Hakuna mshindi aliyepatikana katika duru ya kwanza ya uchaguzi kati ya Jocelerme Privert na Edgard Leblanc Fils, rais wa zamani wa baraza la Seneti. Duru ya pili ya uchaguzi, iliofanyika baada ya masaa matatu asubuhi, imempa ushindi mkubwa Jocelerme Privert. Amepata kura nzuri ya wabunge 64 kwa jumla ya wabunge 92 na kura 13 kwa jumla ya Maseneta 22 waliokuwepo katika kikao hicho.

Jocelerme Privert ana majukumu ya kukamilisha mchakato wa uchaguzi ambao umesitishwa kwa sababu ya maandamano makubwa ya upinzani ambao unalaani "mapinduzi ya uchaguzi" yaliofanywa na Michel Martelly.

Haiti bado katika utata?

Kama uchaguzi wa rais wa mpito umeiondoa Haiti katika tishio la kutokua na taasisi katika kipindi cha miezi minne, uchaguzi ulioahirishwa (duru ya pili ya uchaguzi wa urais na wa wabunge) unaonekana kuwa mgumu kwa nchi hii ya Caribbean.

Tume ya mpito la Uchaguzi (CEP), taasisi inayohusika na kuandaa uchaguzi, itarejelewa upya. Kwa sababu wajumbe wake sita kati ya tisa walijiuzulu. Upinzani unaituhumu serikali kuingilia masuala ya kuandaa uchaguzi.

Pesa ni moja ya changamoto: mchakato wa uchaguzi, ambao bado haujakamilika, tayari umegharimu dola milioni 100, ambapo kiwango kikubwa cha pesa hizo kimetolewa na jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.