Pata taarifa kuu
VENEZUELA

Kampeni za Urais zatamatika nchini Venezuela

Wagombea wa nafasi ya Urais nchini Venezuela wametamatisha kampeni zao kwa hisia kali huku Rais wa Mpito Nicolas Maduro akimwaga machozi na kuahidi kutekeleza sera ya kimapinduzi iliyoasisiwa na marehemu Hugo Chavez.

Rawlins
Matangazo ya kibiashara

Katika kampeni zake Rais wa mpito Maduro ametumia muda mwingi kurejerea ahadi zilizotolewa na marehemu Chavez kwa wananchi na kusema wao watahakikisha wanaendeleza.

Kampeni hizo pia zilifungwa na Kiongozi wa Upinzani Henrique Capriles ambaye alionesha hisia kubwa na kusema atahakikisha analeta mabadiliko makubwa akipatiwa nafasi ya kuongoza Taifa hilo.

Capriles ambaye aliangushwa na marehemu Chavez kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka jana amehimiza wananchi kufanya maamuzi sahihi kwa kumchagua ili Taifa hilo lilweze kupata maendeleo.

Maelfu ya wananchi wamehudhuria kampeni hizo zilizopambwa na shamrashamra nyingi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi siku ya jumapili ambao utaamua nani atakayemrithi Kamanda Hugo Chavez.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.