Pata taarifa kuu
VENEZUELA

Maombolezo ya kifo cha Hugo Chavez yaendelea nchini Venezuela

Wananchi wa Venezuela wameanza siku saba za kitaifa za maombolezo ya kifo cha Rais wa Taifa hilo Hugo Chavez aliyekumbwa na umauti baada ya kuugua maradhi ya Saratani kwa takribani miaka miwili. Mwili wa Chavez utalazwa ikulu ya nchi hiyo ambapo Raia wamepewa muda wa kutoa heshima zao za mwisho mpaka wakati wa Mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mamia kwa maelfu ya raia wa Taifa hilo wamepeperusha bendera zenye picha ya Chavez kama ishara ya maombolezo kwa kifo chake.

Baadhi ya Marafiki wa Karibu wa Chavez wamewasili nchini Venezuela wakijiandaa kwa Shughuli za mazishi wakiwemo Viongozi wa Argentina, Uruguay na Bolivia, huku Mshirika wake wa karibu, Cuba akitangaza kipindi cha Maombolezo ikiwa ni heshima kwa Chavez ambaye ameinua uchumi wa Cuba kwa kuwauzia mafuta kwa bei rahisi na Biashara nafuu ya kibenki.

Chavez alikuwa akipata matibabu ya Saratani baada ya kuwa nchini Cuba kwa kipindi cha miezi miwili, ambapo mwezi Desemba mwaka jana alifanyiwa upasuaji kwa mara ya nne.

Uchaguzi mpya unatarajiwa kuandaliwa ndani ya siku thelathini, wakati makamu wa Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro ambaye anashikilia nafasi hiyo kwa muda akitarajia kupambana na Henrique Capriles ambaye aliangushwa na Hugo Chavez katika uchaguzi wa mwezi oktoba mwaka jana.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.