Pata taarifa kuu
MAREKANI-CORONA-AFYA

Raia 40 wa Marekani waambukwiza virusi vya Corona katika meli ya “Diamond Princess”

Marekani imewarudisha nyumbani raia wake, waliokuwa wamekwama ndani ya Meli, iliyokuwa na watu walioambukizwa na virusi vya Corona nchini Japan, wakati huu, idadi ya watu waliopoteza maisha, ikiongezeka na kufikia zaidi ya 1,700.

Abiria walio kuwa katika Meli "Diamond Princess", wakiingia katika ndege mbili zilizokodiwa na Merika kwenye Uwanja wa ndege wa Haneda huko Tokyo, Februari 17, 2020
Abiria walio kuwa katika Meli "Diamond Princess", wakiingia katika ndege mbili zilizokodiwa na Merika kwenye Uwanja wa ndege wa Haneda huko Tokyo, Februari 17, 2020 REUTERS/Athit Perawongmetha
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, ndege mbili zilizowabeba raia wa Marekani, waliokuwa ndani ya meli hiyo iliyokuwa imetengwa, zimeondoka katika uwanja wa Haneda jijini Tokyo nchini Japan.

Wamarekani waliokuwa ndani ya meli hiyo iliyokuwa imezuiwa, walikuwa 400, na wamekuwa katika hali hiyo tangu tarehe 3 mwezi Februari.

Katika hatua nyingine, licha ya maafisa nchini China kusema kiwango cha maambukizi kinapungua, inaripotiwa kuwa idadi ya watu waliombukizwa virusi hivyo kufikia siku ya Jumatatu ni zaidi ya 70,500.

Idadi kubwa ya maambukizi hayo, yanasalia katika mji wa Wuhan katika jimbo la Hubei, wakati huu Shirika la Afya Duniani, WHO, likisema kwa sasa ni vigumu kueleza ni lini maambukizi haya yatafika mwisho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.