Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-WFP-NJAA-UKAME

WFP yaonya kutokea baa la njaa kufuatia ukame Sudani Kusini

Shirika la kimataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limeonya kuwa hali mbaya ya ukame ambayo inashuhudiwa nchini Sudani Kusini huenda ikasababisha baa la njaa nchini humo katika kipindi cha miezi michache ijayo.

Nchi nyingi barani Afrika zinakumbwa na Ukame, hapa ni Sudani, jirani na Sudani Kusini.
Nchi nyingi barani Afrika zinakumbwa na Ukame, hapa ni Sudani, jirani na Sudani Kusini. (Photo : Jean Pouget/ IRD)
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Wakimbizi, UNHCR, karibu watu milioni moja wameathiriwa na mafuriko ambayo yamefunika maeneo mengi ya miji hali inayozidisha madhila kwa araia ambao tayari wameathirwa na vita vilivyodumu kwa miaka 6.

WFP inasema watu milioni 5 na laki 5 wanatarajiwa kukumbwa na njaa ifikapo mwaka 2020, kipindi ambacho wananchi wengi walitegemea kunufaika na mavuno ya mazao ya mwezi Octoba na Novemba kama ilivyokuwa mwaka jana.

Mafuriko yameharibu karibu tani elfu 73 za mazao yaliyokuwa yavunwe pamoja na mamia ya ng’ombe na mbuzi ambao walikuwa wakitegemewa na familia nyingi.

WFP inasema kwa sasa inahitaji kiasi cha dola za Marekani milioni 270 katika kipindi cha nusu mwaka wa 2020 kukabiliana na hali ya ukame.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.