rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Tabia nchi Mazingira

Imechapishwa • Imehaririwa

Viongozi wa Afrika wawasilisha ripoti yao kuhusu vita dhidi ya tabia nchi

media
Idriss Déby, Rais wa Chad, akiongea katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu tabia nchi Septemba 23, 2019. © REUTERS/Carlo Allegri

Mkutano wa kilele uliyoitishwa Jumatatu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York ulikuwa fursa kwa wakuu wa nchi za Afrika kuwasilisha tathmini ya sera yao ya vita dhidi ya tabia nchi.


Marais hao wameonya kwamba nchi ambazo hazijaendelea sana ndizo zinatishiwa zaidi, na mara nyingi nchi hizo ndizo zinazoathirika zaidi na hali hiyo.

Kwa sehemu kubwa, viongozi wa Afrika ambao walihutubia katika mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New York Jumatatu wiki hii waliwasilisha ripoti zinazofanana. Kila mmoja aliwasilisha orodha ya hatua zilizochukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi au kupanua misitu, kama vile nchini DRC, Gabon, Ethiopia au Congo-Brazzaville, kwa mfano; kusitisha katika kipindi kifupi au cha kati mitambo ya dizeli au ya makaa ya mawe, na kuharakisha mchakato kuelekea uzalishaji wa nishati safi katika miaka kumi au ishirini, kama vile nchini Djibouti, Shelisheli au Nigeria.

Lakini wote, ispokuwa rais wa Sierra Leone, wamesisitiza jambo moja: nchi masikini pia ndizo zinazotishiwa zaidi. Na Afrika iko mstari wa mbele.

Rais wa Chad Idriss Déby alisisitiza mipango ya Chad katika maeneo ya nishati, kilimo na upunguzaji wa gesi chafu, miongoni mwa mengine. Lakini pia ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kutoa msaada mkubwa kwa juhudi za nchi za Kiafrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, ambazo hazihusiki kwa kiwango kikubwa.

Wakati huo huo mwanaharakati wa mazingira Greta Thunberg msichana wa mwenye umri wa miaka 16 kutoka Sweden, amewahotubia viongozi wa dunia, katika Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York, na kuwaambia kuwa wameiangusha dunia kwa kutochukua hatua zaidi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akizungumza kwa hisia mbele ya viongozi wa dunia, mwanaharakati huyo amewashtumu viongozi wa dunia kwa kuendelea kutoa ahadi za uongo wakati huu watu wakiendelea kupoteza maisha na joto kuongezeka kwa sababu ya mabadliko ya hali ya hewa.

Rais wa Marekani Donald Trump aliyeindoa nchi yake katika mkataba wa Paris kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa hakuwepo katika mkutano huo lakini alionekana kwa muda mfupi, katika hadhara iliyokuwepo.