rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Brazili Jair Bolsonaro G7 Emmanuel Macron

Imechapishwa • Imehaririwa

Bolsonaro akubali kupokea msaada wa kifedha kutoka ugenini

media
RAis wa Brazili Jair Bolsonaro akionya mataifa ya G7 kuhusu msaada wao katika kupambana dhidi ya moto wa nyika akatika msitu wa Amazon. REUTERS/Adriano Machado

Hatimaye Brazili imetangaza kwamba iko tayari kupokea msaada wa kifedha " kutoka mashirika ya kigeni na hata nchi za kigeni katika kupambana dhidi ya moto unaoendelea Amazon kwa masharti ya fedha hizo ziwe chini ya udhibiti wa serikali ya Brazili.


Awali serikali ya Brazili ilitangaza kususia msaada wa fedha kutoka nchi za G7 zinazolenga kupambana na moto wa nyika katika msitu wa Amazon.

"Jambo la muhimu ni kwamba fedha hizi, mara zitakapoingia Brazili, zisendi kinyume na uhuru wa Brazil na kwamba usimamizi wa fedha utakuwa chini ya mamlaka yetu," amesema msemaji wa rais. siku moja baada kundi la mataifa yaliyostawi zaidi kiuchumi duniani (G7) kutangaza kuwa ziko tayari kutoa msaada wa milioni 20 kwa kukabiliana na moto wa nyika katika msitu wa Amazon, nchini Brazili.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron - ambaye aliandaa mkutano wa G7 uliofikia tamati Jumatatu - alisema kiasi cha dola milioni 22 kitatolewa.

Dola milioni 22 zilizoahidiwa zinatoka mataifa ya Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Uingereza na Marekani.

Rais Macron alisema pesa hizo zitatolewa haraka iwezekanavyo - ili ziweze kulipia ndege zaidi za zimamoto - na pia Ufaransa itatoa msaada kwa jeshi la Brazil.

Hata hivyo awali mawaziri wa Brazili walisema fedha hizo hazihitajiki na kuyashutumu mataifa hayo yenye nguvu kwa kutaka kuutawala msitu wa Amazon.

Amazon inaangaliwa kimataifa kwa kuwa asilimia 20 ya hewa safi duniani kote inazalishwa kwenye msitu huo.