Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Kisa cha tatu cha maambukizi ya Ebola chathibitishwa mjini Goma

Kesi mpya ya maambukizi ya Ebola imethibitishwa Jumatano jioni, Julai 31, katika mji wa Goma, mashariki mwa DRC, na kufikia idadi ya watu watatu walioambukizwa virusi vya ugonjwa huo hatari katika mji huo wenye wakaazi karibu milioni mbili.

Mtu wa tatu agunduliwa na virusi vya Ebola katika mji wa Goma Julai 31, 2019. (Picha ya kumbukumbu)
Mtu wa tatu agunduliwa na virusi vya Ebola katika mji wa Goma Julai 31, 2019. (Picha ya kumbukumbu) PAMELA TULIZO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mgonjwa wa tatu amegunduliwa na virusi vya Ebola Jumatano mjini Goma, katika mkoa wa Kivu Kusini. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mtu huyo ni binti wa mfanyabiashara wa dhahabu aliyefariki baada ya kuambukizwa ugonjwa jana Jumatano asubuhi.

Marehemu, ambaye alikuwa amewasili katikamji wa Goma Julai 13, aliwekwa chini ya uchunguzi tarehe 22 Julai kabla ya virusi vya Ebola kugundulika nyumbani kwake Julai 30.

Mtu huyo wa tatu aliyeambukizwa virusi vya Ebola anapewa huduma katika vituo vya matibabu, kwa mujibu wa Dk Aaron Aruna Abedi, Mratibu Mkuu wa juhudi za kumaliza ugonjwa huo DRC.

Mlipuko huo uliotangazwa Agosti 1, 2018 katika mkoa wa Kivu Kaskazini na katika Jimbo la Ituri, mashariki mwa DRC, tayari umeua watu 1,803, kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizotolewa Jumatano na mamlaka nchini DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.