Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

Vita dhidi ya Ebola yaendelea mashariki mwa DRC

Wizara ya afya ya nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imesema kuwa katika muda wa siku 21 zilizopita hakuna kisa chochote kilichoripotiwa cha mtu kuambukizwa na virusi hatari vya Ugonjwa wa Ebola, hii ikiwa ni Ishara tosha kwamba Ugonjwa huo wa Ebola umedhibitiwa katika mji wa BENI mashariki mwa nchi hiyo.

Wafanyakazi wa afya wasafirisha mgonjwa katika kituo cha matibabu cha Ebola kilichojengwa na MSF Butembo, Novemba 4, 2018.
Wafanyakazi wa afya wasafirisha mgonjwa katika kituo cha matibabu cha Ebola kilichojengwa na MSF Butembo, Novemba 4, 2018. Photo: John Wessels/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika maelezo yake wakati wa mkutano na waandishi wa Habari hapo siku ya Alhamis, Waziri Oly Ilunga alifahamisha kuwa licha ya kutolewa kwa ripoti hiyo, wananchi wa Maeneo ya Butembo, wameombwa kukaa na tahadhari,

“ Zimepita siku 21 bila ya kuwepo kisa chochote kipya mjini Beni kama mnavyofahamu mapambano yetu yalianzia Beni mwezi Septemba-Oktoba-na Novemba, yaani siku 21 kupita bila ya kujitokeza kisa cha ugonjwa huo mjini Beni inaonyesha kazi kubwa imefanyika katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, na tunaipongeza.

“Ugonjwa wa Ebola sasa umedhibitiwa Mangina, Tshomya, Komanda na Beni: Nguvu zetu za mpambano zimeelekezwa Butembo na maeneo ya Katwa, ” amesema Waziri wa Afya wa DRC Oly Ilunga.

Mapema mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilisema mlipuko wa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni wa pili kwa ukubwa duniani na umeathiri zaidi watoto.

UNICEF ilisema kati ya watu 740 waliothibitishwa kuugua ugonjwa huo, asilimia 30 ni watoto.

UNICEF pia ilisema mlipuko huu ni wa 10 kutokea nchini DRC na ni mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo na ni wa pili kwa ukubwa kuwahi kushuhudiwa kwenye historia ukiongozwa na mlipuko wa ebola huko Afrka Magharibi kati ya mwaka 2014-2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.