Pata taarifa kuu
NEW-ZEALAND-MAJANGA ASILI

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.2 lapiga kaskazini mwa New Zealand

Tetemeko la ardhi lenye la ukubwa wa 6.2 katika vipimo vya Richter limepiga leo Jumanne asubuhi kaskazini mwa kisiwa cha New Zealand, shirika la Marekani linalohusika na masuala ya majanga asili (USGS) limebaini.

Barabara imefungwa baada ya kutokana na maporomoko ya udongo, baada ya tetemeko kubwa la ardhililopiga lilipiga New Zealand  Novemba 14, 2016.
Barabara imefungwa baada ya kutokana na maporomoko ya udongo, baada ya tetemeko kubwa la ardhililopiga lilipiga New Zealand Novemba 14, 2016. Sgt Sam Shepherd/Courtesy of Royal New Zealand Defence Force
Matangazo ya kibiashara

Kitovu cha tetemeko hilo kimegunduliwa kwenye urefu wa kina wa kilomita 228, karibu kilomita 63 mashariki mwa mji wa New Plymouth upande wa magharibi wa kisiwa.

Hakuna hasara yoyote iliyotokea wala dalili zozote za Tsunami kwa mujibu wa USGS.

Kisiwa cha New Zealand kimekuwa kikikabiliwa na majanga ya asili, na hali hiyo imekuwa ikisababisha uharibifu mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.