Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-KIPINDUPINDU-AFYA

Kipindipindu chaua watu ishirini na nne Zimbabwe

Ugonjwa wa kipindupindu nchini Zimbabwe umeenea kutoka mji mkuu Harare hadi sehemu kadhaa za nchi na umeua watu wasiopungua 24 tangu wiki iliyopita, kulingana na ripoti mpya rasmi iliyotolewa leo Alhamisi, ripoti ambayo imebaini kwamba kunaripotiwa uhaba wa dawa.

Wagonjwa wanasubiri matibabu ya ugonjwa wa kipindupindu katika hospitali huko Harare, Zimbabwe, Septemba 11, 2018.
Wagonjwa wanasubiri matibabu ya ugonjwa wa kipindupindu katika hospitali huko Harare, Zimbabwe, Septemba 11, 2018. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

ipoti ya awali ilibaini kwamba Kipindupindi kiliua watu 21.

"Jumla ya vifo 24 vimeoodheshwa tangu mlipuko huo kuanza", ikiwa ni pamoja na 23 huko Harare na moja katika wilaya ya Masvingo, kusini mwa Zimbabwe, kulingana na ripoti ya pamoja ya Wizara ya Afya ya Zimbabwe na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hali ni ngumu kutokana na uhaba wa dawa, maji ya ndani na nguo za kinga, kwa mujibu wa chanzo hicho.

"Dawa zinazohitajika zinapaswa kununuliwa haraka wakati kabla ya mambo kuanza kuwa magumu zaidi ," ripoti hiyo imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.