Pata taarifa kuu
UN-USALAMA-UTAPIA MLO

UN: Watoto milioni mia moja na hamsini wakabiliwa na utapia mlo duniani

Raia wengi barani Afrika wanakabiliwa na tatizo la utapia mlo, na hali hiyo husababisha nchi kurudi nyuma kimaendeleo katika nyanja mbalimbali.

Ukosefu wa lishe na umasikini katika maeneo ya vijijini ni sababu kubwa katika kuenea magonjwa mbalimbali.
Ukosefu wa lishe na umasikini katika maeneo ya vijijini ni sababu kubwa katika kuenea magonjwa mbalimbali. Melanie Stetson Freeman/The Christian Science Monitor/Getty
Matangazo ya kibiashara

Watoto milioni mia moja na hamsini wanakabiliwa na utapia mlo duniani na miongoni mwao milioni 28 ni kutoka kanda ya mashariki na kusini mwa Afrika.

Umoja wa Mataifa unasema bado kuna athari kuhusu maendeleo  kielimu kwa watoto na maendeleo ya nchi mbalilimbali.

Akizungumza Jumanne hii mjini Bujumbura wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kimataifa kuhusu lishe kama nguzo ya maendeleo, mwakilishi wa taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Burundi Garry Conille, amesema “kwa jumla raia wanaishi katika matatizo ya utapia mlo yanayo athiri maendeleo ya nchi zetu”.

Kwa upande wake makamu wa pili wa rais wa Burundi Joseph Butore, ambaye amewakilisha serikali ya Burundi katika mkutano huo amesema kuwa licha ya juhudi kufanyika, idadi ya watu wanaokabiliwa na utapia mlo bado inaendelea kuongezeka.

“Sababu muhimu ni familia kutopata uwezo wa rasili mali, uhaba wa mitaji ya kifedha na kibinadamu, pamoja na hali ya kijamii na kiuchumi na kisiasa. Licha ya juhudi zinazofanyika, idadi ya wanaokabiliwa na utapia mlo bado iko juu katika nchi za bara la Afrika”.

Intro Margeret

Hata hivyo, bado kuna viongozi ambao wana matumaini ya kukabiliana na hali hii.

Margeret Agama Anyetei, mwakilishi wa Umoja wa Afrika amesema “kwa ushirikiano na benki ya Afrika kwa ajili ya maendeleo, Umoja wa Afrika unatakiwa kuanda mkakati wa kukabiliana na aina yoyote ya utapia mlo kwenye bara hili”.

“Afrika yenye ushirikiano, inayojikita na maendeleo na yenye amani ambako raia wake wana afya nzuri inawezekana; tunaweza kufikia Afrika tunayoihitaji, ” Margeret Agama Anyetei ameongeza.

Mkutano huu wa siku tatu sasa itakuwa fursa ya kuafiki kuhusu mikakati ya kukabiliana na hali hii ya utapia mlo katika nchi za bara la Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.