rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Afya

Imechapishwa • Imehaririwa

Ugonjwa wa Kipindupindu waua watu 104 Mbuji Mayi

media
Ugonjwa wa Kipindupindu wasababisha vifo vingi Kasia Mashariki, DRC Wikimedia Commons

Kesi mia nane na thelathini na tatu za kipindupindu ikiwa ni pamoja na vifo 104 vimeripotiwa ndani ya miezi minne katika mji wa Mbuji-Mayi, amesema Alphonse Ngoyi Kasanji, gavana wa jimbo Kasai mahariki, nchini DRC.


Ugonjwa wa kipindupindu umeendelea kusambaa katika wilaya zote za mji huo na kusababisha vifo.

"Hali hii inatokana na ukosefu wa maji katika baadhi ya maeneo na sheria zisizozingatia usafi katika maeneo mengine ya jiji. Serikali ya mkoa imeanzisha harakati za kutokomeza janga hili, lakiniuwezo wake bado ni mdogo dhidi ya changamoto mbalimbali kuanzia kuzuia hadi huduma kwa wagonjwa, "amesema Alphonse Ngoyi.

Gavana wa Kasaï Mashariki ametoa wito kwa washirika wa kiufundi, wa kifedha na wa kibinadamu kusaidia, kutokana na kusambaa kwa haraka kwa janga hili. Amewataka wakaazi wa Mbuji-Mayi kuheshimu kanuni za usafi.

Bw Ngoyi amewataka viongozi wa Regideso, Mamlaka ya maji, viongozi wa mamlaka ya Nishati katika jimbo la Kasai (ENERKA) na MIBA Foundation kushirikana ili wakaazi wa mji wa Mbuji-Mayi wapewe huduma ya maji safi ya kunywa.