rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Ebola Afya

Imechapishwa • Imehaririwa

WHO: Tutahakikisha maambukizi ya Ebola yanatokomezwa DRC

media
Shirika la Afya Duniani (WHO) linaendele kutoa chanjo kwa wakazi wa Mbandaka, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mei 21, 2018. REUTERS / Kenny Katombe

Shirika la Afya Duniani WHO limesema, maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola yatatokomezwa hivi karibu Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hivi karibuni.


Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebre yesus amesema kuna matumaini makubwa sana ya kumaliizka kwa maambukizi hayo kutokana na jitihada za maafisa wa afya nchini DRC na wale wa Shirika hilo.

Awali shirika la Afya Duniani WHO linasema mlipuko wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo haujafika kiwango cha kutangazwa hali ya dharura inayozusha wasiwasi wa kimataifa.

Ebola ni ugonjwa unaoambukiza unaosababisha kuvuja damu ndani ya mwili na mara nyingi waathiriwa hufariki.

Unaweza kusambaa kwa haraka kwa kugusa maji maji yanayotoka mwilini mwa muathiriwa, na mara nyingi dalili za kwanza za ugonjwa huo zilizo kama homa ya kawaida siyo rahisi kuzitambua.

Ugonjwa wa Ebola umesababisha watu 27 kupoteza maisha na wengine kuambukizwa tangu mwezi uliopita.