Pata taarifa kuu
WHO-TUMBAKU-AFYA

WHO: Matumizi ya tumbaku yamepungua lakini bado kuna hatari

Wakati Dunia ikiadhimisha Alhamisi hii Mei 31, siku ya kupinga matumizi ya tumbaku, Shirika la Afya Duniani, WHO, linasema matumizi ya tumbaku yamepungua lakini bado kuna hatari.

Matumizi ya tumbaku yanadhuru binadamu.
Matumizi ya tumbaku yanadhuru binadamu. REUTERS/Christian Hartmann/Illustration
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ripoti ya WHO, idadi ya wanaume wenye umri wa miaka 15 wanaotumia tumbaku imepungua kutoka asilimia 43 mwaka 2000 hadi asilimia 34 mwaka 2015.

Kupitia ripoti yake iliyotolewa leo, WHO inasema matumizi hayo yamepungua kutoka asilimia 27 mwaka 2000 hadi asilimia 20 mwaka 2015.

Halikadhalika kwa wanawake ni kutoka asilimia 11 mwaka 2000 hadi asilimia 6 mwaka 2015, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani.

Hata hivyo WHO inasema kupungua kwa matumizi ya tumbaku hatoshelezi kufikia lengo linalotakiwa la kuepusha watumiaji wa tumbaku kupata magonjwa ya moyo na magonjwa mengine ya kuambukiza.

WHO inasema bado kuna tishio kwa kuwa watu wengi hawafahamu uhusiano kati ya kuvuta tumbaku na magonjwa ya moyo.

Mkurugenzi wa WHO anayehusika na magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs) Dkt Douglas Bettcher, matumizi ya tumbaku yanaduru.

Watu wengi duniani hasa barani Afrika na katika nchi ambazo hazijaendelea hawa uelewa wowote kuhusu madhara ya matumizi ya tumbaku. Lakini baadhi, ambao ni wachche wanafahamu kuwa matumizi ya tumbaku yanaua

Zaidi ya watu milioni 17.9 hufariki dunia kila mwaka kutokana na matumizi ya tumbaku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.