rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Ebola Afya

Imechapishwa • Imehaririwa

WHO: Kuna hatari maambukizi ya Ebola kuendelea kuenea DRC

media
Licha ya hatua kadhaa za kukabiliana na Ebola, visa vipya vimekua vikigunduliwa nchini DRC. REUTERS/Media Coulibaly

Shirika la Afya Duniani WHO limesema kuwa mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo una hatari ya kuendelea kuenea wakati huu likisema kuwa linalenga kuwapa chanjo watu zaidi ya elfu 10.


Mkuu katika kitengo cha dharula cha WHO Peter Salama, amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa virusi hivi kuenea katika siku chache zijazo kutokana na changamoto ambazo zimejitokeza za watu kukimbia hospitalini.

Haya yanajiri wakati huu kukiripotiwa kuwa raia waliokuwa na virusi vya Ebola na ambao walikimbilia kanisani kufanya maombi, wamefariki dunia hali inayozusha hofu zaidi ya kuenea kwa maambukizi haya.

Watu zaidi ya 27 wamethibitishwa kupoteza maisha mpaka sasa kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola huku wengine zaidi ya 40 wakithibitishwa kuwa na maambukizi.