rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Ebola Afya

Imechapishwa • Imehaririwa

Imani potufu zatatiza zoezi la utoaji chanzo dhidi ya Ebola DRC

media
Virusi vya Ebola. CDC/Frederick A. Murphy

Wakati huu zoezi la utoaji chanzo kudhibiti maambukizi ya virusi hatari vya ugonjwa wa Ebola likiendelea nchini DRC, wafanyakazi wa afya wanakabiliwa na changamoto kutokana na kukosa watu kwenye baadhi ya maeneo kunakosababishwa na imani za kishirikana.


Baadhi ya watu wanakataa kupatiwa matibabu na badala yake wanageukia kwa wachungaji na kufanya maombi ili kuundoa ugonjwa wa Ebola wanaoamini umeletwa kutokana na laana na matokeo ya imani za kishetani.

Juma moja lililopita mchungaji mmoja alifariki dunia baada ya kumfanyia maombi mgonjwa aliyekuwa na maambukizi ya Ebola.

Mmoja wa wauguzi wanaoshiriki katika zoezi la utoaji wa chanjo hiyo amesema kuwa raia wengi wamewakatalia kupewa matibabu na badala yake wanaishia kufanya maombi.

Tangu kuripotiwa kwa ugonjwa huo Mei 8 kwenye eneo la Bikoro jumla ya watu zaidi ya 27 mpaka sasa wameelezwa kupoteza maisha kutokana na virusi vya ugonjwa wa Ebola.

Serikali ya DRC inasema imani potofu kwa wananchi walioko kwenye eneo la Bikoro na mji wa Mbandaka zimeendelea kuwa changamoto katika mapambano dhidi ya kuenea kwa virusi hivyo.