rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC WHO Afya Ebola

Imechapishwa • Imehaririwa

WHO: Tuko tayari kukabiliana na Ebola DRC

media
Licha ya hatua kadhaa za kukabiliana na Ebola, visa vipya vimekua vikigunduliwa nchini DRC. REUTERS/Baz Ratner

Jumla ya visa 30 vya ugonjwa wa Ebola vimeripotiwa nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kwa mujibu wa shirika la afya Duniani WHO. Ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu watatu.


Waliokufa ni pamoja na mwanamume wa umri wa miaka 39 aliyetajwa kuwa "mgonjwa sufuri" na watu wawili ambao walikuwa wamekaribiana naye, WHO ilisema.

Shirika la Afya Duniani, WHO limeahidi kuchukua hatua za tahadhari na za haraka, ili kuzima mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola kaskazini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

WHO inasema kuwa wataalamu wake wa kiufundi, wametumwa hadi maeneo ya vijijini, kunako aminika kutokea visa 11 vya ugonjwa wa Ebola -- zikiwemo ripoti ya vifo vya watu watatu.

WHO imesema wiki hii litatuma dozi 4,000 ya njano ya ugonjwa hatari wa Ebola Kaskazini Magharibi mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hatua hii inakuja baada ya ziara ya Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ambaye mwishoni mwa wiki alizuru DRC.

Tangu Aprili 4 nchini Congo, kumeripotiwa zaidi ya visa 30 ambavyo huenda ni vya ugonjwa wa Ebola - ikiwemo vifo vya watu 18 - licha ya kwamba ni visa viwili tu vilivyothibitishwa kutokana na Ebola.

Ebola unaweza kusambaa kwa kasi kupitia kugusa maji maji ya kutoka mwilini mwa muathiriwa. Dalili za kwanza zinazokuja kwa mfano wa homa sio rahisi kuzitambua.

Virusi vya Ebola vimegunduliwa katika miaka ya nyuma mnamo 1976 katika milipuko miwili ambapo watu 151 walifariki katika enoe la Nzara, Sudan kusini na watu 280 waliofariki katika eneo la Yambuku karibu na mto Ebola uliopewa jina kutokana na ugonjwa huo.

Kuna aina tano ya virusi vilivyotambuliwa vya Ebola, na kilicho hatari zaidi ni kile cha Zaire (DRC).

Na ndicho kirusi kilichotambuliwa katika mlipuko wa sasa huko Congo ambapo sasa kuna chanjo ilio tayari kwa matumizi ya dharura.

Mlipuko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo utakuwa changamoto kwa maafisa walio katika eneo hilo.

Lakini pia ni changamoto na ni fursa kwa jumuiya ya kimataifa kuthibitisha kwamba imejifunza kutokana na janga la Afrika magharibi.

Huu ni mlipuko wa 8 uliotambuliwa wa Ebola nchini Congo, tangu kisa cha kwanza kutambuliwa cha Ebola nchini humo mnamo mwaka wa 1976.