rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Ebola Afya WHO

Imechapishwa • Imehaririwa

Visa vipya vya Ebola vyaibuka DRC

media
Ugonjwa wa Ebola waripotiwa kaskazini magharibi mwa DRC. appsforpcdaily.com

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kwamba visa vipya vya ugonjwa wa Ebola vimeibuka kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.


Kwa mujibu wa chanzo cha wizara ya Afya watu 17 walifariki dunia baada ya kuonekana kuwa waliokua nazo ni kama zile za watu walioambukizwa virusi vya Ebola, na tayari Kuna visa viwili abavyo vimethibitishwa

Shirika la afya duniani (WHO) limesema tangazo la kuzuka kwa visa hivyo vipya limetolewa baada ya matokeo ya uchunguzi wa maabara kuthibitisha visa viwili vya Ebola kati ya sampuli za wagonjwa watano waliokuwa wanashukiwa.

Shirika hilo la afya duniani linasema limetoa $ milioni 1 kutoka fuko la dharura na limetuma zaidi ya wataalamu 50 kufanya kazi na maafisa nchini Congo.

Kwa mujibu wa chanzo cha serikali madaktari wakiwemo na wataalam wa maradhi ya Ebola kutoka wizara ya afya nchini wakiambatana na wale wa shirika la afya duniani (WHO) leo Jumatano wanatarajia kwenda katika jimbo la Equateur baada ya kuthibitishwa kuwepo ugonjwa huo.

Nchi ya DRC katika miaka ya hivi karibuni ilikumbwa na ugonjwa wa Ebola ambapo watu kadhaa walifariki dunia.

Virusi vya ugonjwa huo viligunduliwa kwa mara ya kwanza katika nchi hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Zaire.

Ugonjwa huu ulisababisha maafa makubwa katika nchi za Afrika Magharibi hasa nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia ambapo watu 11,000 walifariki dunia.