rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

India Majanga ya Asili

Imechapishwa • Imehaririwa

Mvua zaua watu zaidi ya 78 nchini India

media
kijiji kidogo cha jimbo la Rajasthan, India ambapo watu zaidi ya 78 wamepoteza maisha kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Vincent Desjardins

Mvua kubwa zimeua watu wasiopungua 78 kaskazini na magharibi mwa India, serikali ya nchi hiyo imetangaza. Watu wengi wamepoteza makazi yao kutokana na mvua hizo zinazoendelea nchini humo.


Watu thelathini na watatu walipoteza maisha siku ya Jumatano wiki hii katika jimbo la magharibi la Rajasthan na wengine 45 walipoteza maisha katika jimbo la Uttar Pradesh, kaskazini mwa nchi.

"Tumekumbwa na mvua kubwa yenye upepo usio wa kawaida hali ambayo ilisababisha watu 33 kupoteza maisha katika maeneo ya Alwar, Dholpur na Bharatpur, katika jimbo la Rajastan" amesema Hemant Gera, Afisa wa Idara ya huduma za dharura katika jimbo la Rajasthan.

Mvua hizo pia zimeathiri maeneo ya Saharanpur, Bareilly, Bijnore na Agra katika jimbo la Uttar Pradesh.