Pata taarifa kuu
MAREKANI-TABIA NCHI-MAZINGIRA

Bloomberg atoa dola milioni 4.5 kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa

Meya wa zamani wa jiji la New York nchini Marekani Michael Bloomberg amesema atalipa Dola Milioni 4.5 katika mchango wake kuhakikisha kuwa mkataba wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa unatekelezwa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto), Anne Hidalgo (kulia) na Michael Bloomberg (katikati).
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kushoto), Anne Hidalgo (kulia) na Michael Bloomberg (katikati). REUTERS/Christophe Petit Tesson
Matangazo ya kibiashara

Pesa hizo ni zitasaidia UNFCC kutekeleza majukumu yake kwendana na mkataba wa Paris.

Tajiri huyu muhisani na meya wa zamani wa jiji la New York, Juni mwaka jana aliahidi kujaza pengo la fedha la idara hiyo lililosababishwa na hatua ya rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza kujiondoa kutoka kwenye mkataba wa Paris kuhusu tabianchi wa mwaka 2015.

Bloomberg amesema yeye binafsi ana jukumu la kuhakikisha kuwa, mazingira yanaimarishwa na amechukua hatua hiyo baada ya rais Donald Trump kuonekana kutounga mkono mkataba huo na kujiondoa mwaka uliopita.

Mchango wa Bloomberg utasaidia katika operesheni za ujumla kama vile kusaidia nchi kufikia malengo yake  ya kupunguza gesi za viwandani kwendana na makubaliano yaliyofikiwa na mataifa 193 katika mji mkuu wa Paris nchini Ufaransa.

Nae Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter, amemsifu Michael Bloomberg sio tu kwa uhisani wake kwa Umoja wa Mataifa lakini pia kuwa mstari wa mbele kuhusu msuala ya mabadiliko ya tabianchi duniani.

Mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa, unataka mataifa 187 kuhakikisha kuwa kiwango cha joto hakivuki sentigredi 2 hasa kutoka kw a mataifa yenye viwanda vikubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.