rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufilipino Rodrigo Duterte

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais wa Ufilipino aamuru kufungwa kwa kisiwa cha Boracay

media
Utalii kwenye kisiwa kidogo cha Boracay, (picha), Ufilipino umepigwa marufuku kwa muda wa miezi zaidi ya sita, kutokana na uchafu unaokikabili. REUTERS/Charlie Saceda

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameamuru kufungwa kwa kisiwa kidogo cha Boracay, ambacho alielezea mwezi wa Februari kuwa ni "shimo lililojaa uchafu", na hivyo kutaka kisiwa hicho kifanyiwe ukarabati.


Tangazo hilo lilitolewa siku ya Jumatano usiku kwenye Twitter na msemaji wa rais, agizo ambalo litaanza kutumika tarehe 26 Aprili na kwa muda wa zaidi ya miezi sita, hadi Oktoba 25.

Shirika za ndege nchini Ufilipino zimekua za kwanza kufuta safari za kila siku kuelekea eneo hilo la kivutio kwa watalii, kilomita 300 kusini mwa Manila.

Kisiwa cha Boracay kinachojulikana kwa fukwe zake za mchanga mweupe, klabu za usiku na michezo ya baharini, kilipelekea watalii milioni 2, hasa kutoka China, Korea Kusini, Marekani na Australia kuwasili eneo hilo mwaka jana.

Kisiwa hicho kina biashara 1,800 na wengi wao humwaga maji taka katika bahari, kinyume na kanuni, kulingana na Wizara ya Mazingira ya Ufilipino ambayo imekua imeomba kisiwa hicho kufungwa kwa mwaka mmoja.