rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa
  • Mafuriko yameua watu kumi na nane Iran (idara ya hali ya Dharura)

Zambia Edgar Lungu

Imechapishwa • Imehaririwa

Serikali ya Zambia yadhibiti maradhi ya kipindupindu

media
Hospitali kuu ya Lusaka, Zambia, ambako wagonjwa wengi wanaendelea kuhudumiwa. DAWOOD SALIM / AFP

Shule, makanisa na masoko yamefunguliwa tena baada ya kufungwa kwa muda wa wiki tatu, kutokana na janga la kipindupindu nchini Zambia.


Serikali ilikuwa imezuia mikutano ya watu, kwa hofu ya kusambaa kwa ugonjwa huo hatari.

Kipindupindu kimesababisha vifo vya zaidi ya watu 70 nchini humo tangu mwezi Septemba mwaka uliopita.

Mwishoni mwa wezi Desemba 2017, Rais Edgar Lungu wa Zambia, aliamuru vikosi vya kijeshi na polisi wasaidiane na maafisa wa matibabu katika kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu ambacho tayari kilisababisha vifo vya watu zaidio ya 41 katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

Mwanzoni mwa mwezi Januari Wizara ya Afya ya Zambia ilitangaza kuwa, maambuzi ya kipindipindu yameshika kasi kubwa zaidi katika mji mkuu wa nchi hiyo Lusaka.

Taarifa iliyotolewa na maafisa wa serikali ya Zambia ilisema idadi ya watu walioambukizwa maradhi ya kipindupindu ilifika elfu mbili katika mji mkuu wa nchi hiyo Lusaka pekee.