Papa Francis : Ni marufuku kwa uuzaji wa sigara Vatican
Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis amepiga marufuku ya uuzaji wa sigara ndani ya eneo la Vatican. Hatu hii itaanza kutekelezwa mwaka ujao.
Imechapishwa:
Papa Francis ametoa agizo hilo kufuatia takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kwa kusababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka.
Zaidi ya wafanyakazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanaruhusiwa kununua pakiti tano za sigara kila mwezi kutoka kwa duka lisilotozwa ushuru.
Mauzo ya sigara yanakadiriwa kuiletea Vatican mamilioni ya fedha kila mwaka.
Msemaji wa Vatican amesema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubali na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu.
Greg Burke amesema kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu.