rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Madagascar Afya

Imechapishwa • Imehaririwa

Madagascar yaendelea kukabiliana na maradhi ya tauni

media
Timu ya kuzuia dhidi ya maradhi ya tauni katika mitaa ya Antananarivo, Madagascar, Oktoba 10, 2017. RIJASOLO / AFP

Idadi ya watu walipoteza maisha kutokana na maradhi ya tauni nchini Madagascar imefikia watu 124 wakati huu serikali ikifaulu kupunguza ukali wa maradhi hayo kuendelea kutapakaa.


Wizara ya afya hapo jana imesema watu 1.133 wameambukizwa maradhi hayo, miongoni mwao 780 wamepona, huku wengine 290 wakiendelea kupewa matibabu.

Jumla ya watu 63 wamefariki wakiwa Hospitalini wengine 61 wakiwa nyumbani.

Licha ya takwimu hiyo kuonekana kuwa juu, wizara ya afya nchini Madagascar imepongeza hatuwa ya kuzuia maradhi hayo kuendelea kuambukia.

Mkurugenzi wa WHO nchini Madagascar Charlotte Ndiaye amesema wanashirikiana na serikali ya nchi hiyo katika kutoa msaada kwa waathirika wa maradhi hayo.