rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Afya Ebola Marburg

Imechapishwa • Imehaririwa

Uganda yatiwa wasiwasi na mlipuko wa virusi vya Marburg

media
Homa inayosababishwa na virusi vya Marburg iliripotiwa kwa mara ya kwanza miaka 10 iliyopita katika eneo la Kamwenge, magharibi mwa Uganda. Kwenye picha ni wakazi wa eneo la Kamwenge. AFP/File, Michele Sibiloni)

Uganda inakabiliwa na changamoto mpya ya virusi vya Marburg vinavyo ripotiwa mashariki mwa nchi hiyo. Tangu mwezi Septemba uliyopita, watu wawili wamefariki dunia kutokana na virusi hivyo vinavyo uwa kwa haraka kama virusi vya Ebola.


Siku ya jumapili Waziri wa afya wa Uganda Ruth Aceng amethibitilisha kufariki kwa watu wawili kutokana na virusi vya Marburg nchini humo.
Idara ya utafiti wa virusi vya Marburg nchini Uganda imehakikisha kwamba ugonjwa huo unauwa haraka kama Ebola.

Ni homa inayosababisha mgonjwa kutokwa na damu, kutapika na kuendesha na ugonjwa wenye kuambukia haraka. Ugonjwa huo uliripotiwa kwa mara ya kwanza miaka 10 iliyopita katika eneo la Kamwenge, magharibi mwa Uganda.

Waziri Aceng amewataka wakazi wa eneo la Queen kwenye mpaka na Kenya, ambako uganjwa huo unaripotiwa, kuwa makini.

Wizara ya Afya nchini Uganda imeonya dhidi ya mlipuko wa virusi vikali vinavyosababisha ugonjwa wa Marburg katika eneo la Kusini Magharibi mwa nchi.

Katika taarifa ya wizara hiyo, maafisa wamesema kuwa uchunguzi wa maabara ulithibitisha kuwa watu wawili wa familia moja walifariki kutokana na virusi hivyo wilayani Kabale.

Jamaa wengine wa familia hiyo, wanaaminika kufariki kutokana na ugonjwa huo mapema mwezi huu.

Virusi vya Marburg, ambavyo vinaaminika kuwa na dalili sawa na homa ya Ebola na huambukizwa katika njia moja, kupitia majimaji ya mwilini mfano jasho, mate na hata damu pamoja na kuwashika wanyama waliombukizwa na homa hiyo.

Hata hivyo ugonjwa huo hauna tiba.

Virusi vya Marburg vinaweza kumuuwa mtu mwenye afya katika kipindi cha wiki moja tu baada ya kuanza kutapika na kuwa na tumbo la kuendesha na hatimae kutokwa damu ndani kwa ndani.