Pata taarifa kuu
NIGERIA-AFYA

Kipindupindu chaua watu 35 kaskazini mashariki mwa Nigeria

Watu thelathini na tano wamefariki dunia kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kaskazini mashariki mwa Nigeria, eneo ambalo linathiriwa na kuzuka kwa magonjwa ya kuambukiza, kulingana na ripoti mpya ya Wizara ya Afya ya jimbo la Borno siku ya Jumapili.

Wakimbizi katika kambi ya Munguno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, wakabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu
Wakimbizi katika kambi ya Munguno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, wakabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu TRF-Kieran Guilbert
Matangazo ya kibiashara

"Idadi ya vifo ni 35," ilisema taarifa ya wizara, na kuongeza kuwa "idadi ya watu wanashukiwa kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu imefikia 1.283".

Vifo vingi na kesi za watu wanaoshukiwa kuambukizwa zimeorodheshwa katika kambi wakimbizi wa ndani ya Garage Muna, inayowapa hifandhii watu 20,000 ambao walikimbia mauaji ya kundi la boko Haram katika kitongoji cha Maiduguri.

Ripoti ya awali ya Wizara ya Afya ya jimbo la Borno ilibaini kuwa watu 21 walifariki dunia siku ya Jumanne ya wiki hii iliyopita.

Kipindupindu ni ugonjwa unaoambukia na kuambukizwa na bakteria inayopatikana katika maji au chakula.

Jumla ya kesi 775 ziliripotiwa kambini, ambapo wakimmbizi wa ndani wanaishi katika mazingira magumu.

Katika makambi haya, magonjwa yanayotokana na maji ni tishio la mara kwa mara, hasa wakati wa msimu wa mvua, kwa sababu mifumo mibovu ya kusafirisha imekua ikisababisha maji kukaa sehemu moja kwa muda mrefu.

Licha ya jitihada za serikali ya Nigeria, pamoja na mashirika ya kitaifa na ya kimataifa ya misaada, janga hili halingeweza kudhibitiwa na sasa limeenea katika mji wa Dikwa, kilomita 90 kutoka Maiduguri, ambapo kesi 438 zimeorodheshwa.

Katika mji wa Monguno, kilomita 138 kutoka mji mkuu wa jimbi la Borno, uchunguzi umezinduliwa baada ya kesi za watu wanaoshukiwa kuambukizwa ugonjwa huu, kulingana na taarifa hiyo.

Kundi la Boko Haram limesababisha vifo vya watu zaidi ya 20,000 na watu milioni 2.6 walitoroka makazi yao, ambapo wengi wao wanaishi katika kambi zisizo salama kwa chakula na afya kama kipindiupindu na malaria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.