Pata taarifa kuu
MAREKANI-ANGA

Marekani kupatwa kwa Jua Jumatatu hii

Mamilioni ya watu nchini Marekani wanatarajia kushuhudia kupatwa kwa Jua siku ya Jumatatu katika majimbo 14 nchini Marekani.

Picha ya kupatwa kwa Jua iliyoshuhudiwa kutoka pwani ya kisiwa cha Ternate, Indonesia, Machi 9, 2016.
Picha ya kupatwa kwa Jua iliyoshuhudiwa kutoka pwani ya kisiwa cha Ternate, Indonesia, Machi 9, 2016. REUTERS/Beawiharta
Matangazo ya kibiashara

Tukio la kupatwa la tarehe 21 Agosti ni kupatwa kamilifu kwa Jua ambapo Mwezi hufunika sura ya Jua. Watu wachache sana hubahatika kuona Jua lote likifunikwa kwa vile inatakiwa uwe ndani ya eneo la kilomita 100 ambamo, kwa dakika tatu, mchana hugeuka kuwa usiku. Kwa tukio la Agosti 21, eneo la giza litatengeneza mkanda mwembamba utakata nchi nzima ya Marekani kutoka ukingo wa magharibi hadi wa mashariki.

Baadhi wanaona kwamba tukio hili ni la kihistoria na la kujivuni baada ya tukio kama hili kutokea miaka 100 iliyopita. Na wengine hasa waumini mbalimbali wanaona kuwa tukio hili ni dalili za mwisho wa dinia.

Tukio la Agosti 21 limekuja kujulikana kama “Tukio Kabambe la Kupatwa Marekani” na hiyo imeenea duniani kote kwa mtandao. Kuna habari potofu pia zinasambazwa kwamba Dunia nzima litakuwa na giza siku hiyo ya Agosti 21, ambayo si kweli hata kidogo. Giza litaonekana katika mkanda mwembamba utakao kata nchi ya Marekani na kwa dakika tatu tu.
Muda wa kupatwa ni kati ya saa 12:46 jioni ya Agosti 21( saa za Afrika Mashariki), hadi saa 6:05 usiku saa za Afrika Mashariki. Mviringo mweusi wa Mwezi utaanza kufunika Jua kuanzia saa 1:46 jioni hadi saa 5:02 usiku.

Raia nchini Marekani watashuhudia kupatwa kwa Jua Agosti 21, na hasa sehemu ambazo litapatwa kamilifu, wanaastronomia wamewatayarisha watu kuangalia Jua kwa usalama na kufurahia tukio la ajabu, na wanafunzi kutumia nafasi hii kujifunza elimu ya anga za juu. Matayarisho makubwa yalianza kufanyika miaka miwili kabla ili kuwahimiza watu kusafiri kwenda katika maeneo ya kupatwa kamilifu kwa Jua na kuliangalia kwa usalama kwa kutumia miwani maalum. Kwa wanasayansi, tukio la kupatwa kamilifu kwa Jua ni nafasi pekee ya kupima na kuchunguza tabia za anga ya Jua maana hakuna njia nyingine kuiona kwa uwazi hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.