rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Afya Ukimwi

Imechapishwa • Imehaririwa

Kongamano kuhusu Ukimwi duniani: Wanaharakati waishutumu Ufaransa kwa kutotekeleza ahadi zake

media
Linda Gail-Bekker, rais wa Shirikisho la Kimataifa la Ukimwi, ameonya dhidi ya kutowajibika kifedha katika mapambano dhidi ya Ukimwi. FRANCOIS GUILLOT / AFP

Zaidi ya wanasayasi 6000 kutoka nchi mbalimbali duniani walihudhuria Jumapili hii Julai 23 ufunguzi wa kongamano kuhusu Ukimwi duniani, kongamano ambalo lilifanyika katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Waziri wa Afya wa Ufaransa Agnès Buzyn, ambaye alimuwakilisha rais Emmanuel Macron, alizomelewa.


Wanaharakati mbalimbali nchini Ufaransa walionyesha hasira yao mbelea ya wanasayansi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo, huku wakimshtumu rais wa Ufaransa kuwa miongoni mwa watu wanaochochea maambukizi ya Ukimwi. Wakati ambapo mapambano dhidi ya Ukimwi yakiendelea, itatakiwa kuongeza juhudi, huku ikiarifiwa kuwa fedha za umma kutoka Mfuko wa Global dhidi ya VVU zilipungua mwaka jana.

Wanaharakati hao wamesema uamuzi wa kupunguza uliotangazwa katika utafiti wa Ufaransa na kukosekana kwa Emmanuel Macron wakati wa ufunguzi wa mkutano ni mambo yasiokubalika. Mashirika Coalition Plus, Act- na Aides yameishtumu Ufaransa kwa kutoawajibika kwa ahadi zake. Hata hivyo Waziri wa Afya wa Ufaransa, Agnès Buzyn, alifutilia mbali tuhuma hizo. "Nadhani mapambano dhidi ya Ukimwi hayangelifikia katika hatua hii bila kuwa ya mchango mkubwa wa wanaharakati, kwa hivyo tunawashukuru sana," alijibu Waziri Buzyn, huku akiwataka kujipongeza.

Wanaharakati wanaopambana dhidi ya Ukimwi wamekosoa kauli ya Agnès Buzyn, huku wakibain i kwamba katika kongamano hilo hangeliweza kutangaza bajeti katika masuala ya kupambana na ugonjwa huo. Waandaaji wa kongamano hilo wameitolea wito Marekani, mchangiaji wa kwanza katika mapambano dhidi ya Ukimwi, kuendelea kutoa mchango wake, wakati ambapo rais Donald Trump alitishia kupunguza bajeti katika mapambano dhidi ya Ukimwi. Vinginevyo, hali hii itasababisha vifo zaidi na maambukizi, alionya katika mkutano na waandishi wa habari Linda Gail-Bekker, mtafiti katika kito cha Desmond Tutu HIV nchini Afrika Kusini, na rais wa Shirikisho la Kimataifa la Ukimwi.

Kupunguzwa kwa bajeti katika mapambano dhidi ya Ukimwi inaweza kuharibu jitihada zote zilizofanywa, pia alionya mkuu wa UNAIDS, Michel Sidibé. "Tumeanza kuvunja uti wa mgongo wa janga hili. Ni wakati ambao hatuwezi kuacha kuendelea na jitihada hizi, "alisisitiza.