rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC Afya

Imechapishwa • Imehaririwa

Watu 12 wafariki dunia kufuatia mlipuko wa ugonjwa usiojulikana Nyiragongo

media
Maji safi yamekua haba katika baadhi ya vitongoji vya mji wa Goma. St├ęphanie Aglietti/RFI

Watu 12 wamepoteza maisha baada ya kuanza kuharisha na na kutapika katika kijiji cha Kanyaruchinya eneo la Nyiragongo katika Jimbo la Kivu Kaskazini.


Mashirika ya kiraia yanasema miongoni mwa watu hao walipoteza maisha kuanzia siku ya Ijumaa ni watito saba wenye chini ya umri wa miaka mitano na watu wazima watano.

Watu wengine 120 wamelazwa hopsitalini mjini Goma, wanakopewa matibabu.

Ukosefu wa maji safi ya matumzi ya nyumbani katika maeneo mengi ya jimbo la Kivu Kaskazini, inaelezwa kuwa chanzo cha hali hii.

Serikali ya mjini Goma haijaeleza lolote kuhusu hali hii inayoendelea kushuhudiwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini.