Pata taarifa kuu
UNICEF-WATOTO-HEWA

UNICEF: mtoto mmoja kati ya saba apumua hewa yenye sumu

Watoto milioni mia tatu duniani, sawa na mtoto mmoja kati ya saba, wanapumua hewa yenye sumu kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumatatu hii Oktoba 31 na shirika la Umoja wa Mataifa kwa watoto (Unicef). Unicef itawatolea wito viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka katika nchi zao katika mkutano ujao kuhusu tabia nchi (COP22).

Katika mitaa ya Beijing, wakati wa uchafuzi wa mazingira mwezi Desemba 2015, wazazi wamekua wakisumbuka kwa ajili ya afya ya watoto zao.
Katika mitaa ya Beijing, wakati wa uchafuzi wa mazingira mwezi Desemba 2015, wazazi wamekua wakisumbuka kwa ajili ya afya ya watoto zao. REUTERS/Kim Kyung-Hoon
Matangazo ya kibiashara

Mmoja kati ya watoto saba duniani anakabiliwa na uchafuzi wa mazingira, huo ni mtazamo uliyotolewa na Unicef ambayo inatoa wito kwa viongozi wa dunia, wiki moja kabla ya mkutano kuhusu tabia nchi (COP22) utakaofanyika mjini Marrakech.

"Uchafuzi wa hewa unachangia kwa kiasi kikubwa kwa vifo vya watoto 600 000 walio na umri ulio chini ya miaka mitano kila mwaka na unatishia maisha na hatima ya mamilioni wengine," amesikitika Anthony Lake, Mkurugenzi Mkuu wa Unicef.

Shrika hili la Umoja wa Mataifa kwa watoto linaona kuwa watoto milioni 300 duniani kote wanaishi katika eneo ambalo uchafuzi wa hewa inayotoka nje unazidi mara sita viwango vya kimataifa. Asia ya Kusini ni inaongoza ikiwa na watoto milioni 620 wanaopumu hewa chafu zaidi, ikifuatiwa na Afrika ambapo watoto milioni 520 wanapumua hewa chafu, Asia ya Mashariki na Pasifiki (milioni 450).

Ili kupambana dhidi ya uchafuzi huu, Unicef inapendekeza hatua nne za dharura kwa viongozi wa dunia, ikiwa ni pamoja na kufanya juhudi kubwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ubora hewa kwa kupunguza matumizi ya mafuta na kuendeleza zaidi nishati mbadala. Unicef pia inatoa wito kwa upatikanaji rahisi wa huduma za matibabu kwa watoto, ikiwa ni pamoja na kampeni za chanjo ili kupunguza uwezekano wa kupata kiurahisi ugonjwa wa kupumua.

Unicef pia inapendekeza kwamba vyanzo vya uchafuzi kama viwanda viwekwe mbali na shule, viwanja vya michezo pamoja na urasibu mzuri wa taka. Hatimaye, majiko ya gesi safi huboresha ubora wa hewa katika nyumba, Unicef imesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.