Pata taarifa kuu
UN-HAITI-AFYA

UN yakubali kuwa ni chanzo cha mlipuko wa Kipindupindu Haiti

Kwa mara ya kwanza tangu kutokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, Umoja wa mataifa umekiri kuwa ulichangia kwa mlipuko wa ugonjwa nchini nchini Haiti, uliowaua watu zaidi ya elfu kumi, na wengine 800,000 waliambukizwa miaka sita iliyopita.

Wanaharakati wa haki za binadamu na waathirika wa kipindupindu wakiandamana nje ya makao makuu ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti (MINUSTAH), Oktoba 15, 2015, katika mji wa Port-au-Prince.
Wanaharakati wa haki za binadamu na waathirika wa kipindupindu wakiandamana nje ya makao makuu ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti (MINUSTAH), Oktoba 15, 2015, katika mji wa Port-au-Prince. AFP PHOTO/HECTOR RETAMAL
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti nyingi za kisayansi, askari wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kutoka Nepal ndio walikua chanzo cha ugonjwa huo ambao ulianza kushuhudiwa nchini humo mwezi Oktoba 2010 katika kisiwa Caribbean. Lakini hadi sasa, Umoja wa Mataifa umekua ukikanusha kuhusika kwake.

"Umoja wa Mataifa hatimaye utahitaji uangalifu mkubwa kwa kuwahudumia raia katika mambo ya usalama, baada ya kuhusika kwake katika mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu, hasa ukiangalia mateso waliyoyapata wale walioathirika na ugonjwa huu". Maneno haya yaliandikwa na Farhan Haq, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, huku akibaini kwamba "majibu mapya yatawekwa hadharani katika miezi miwili ijayo, katika uratibu na serikali ya Haiti".

Ushindi kwa maelfu ya Wahaiti

Nchini Haiti, wanasheria wa waathirika wa kipindupindu, ambao kwa miaka mitano wakidai fidia, wamekaribisha kile kinachoonekana kuwa mabadiliko. "Huu ni ushindi mkubwa kwa maelfu ya Wahaiti ambao, ili kutendewa hakii, waliteseka, walisaini nyaraka na hatimaye kuvutana mahakamani na Umoja wa Mataifa," wanasheria hao wamesema katika taarifa yao ya pamoja. "Ni wakati muafaka kwa Umoja wa Mataifa kuonyesha kuwa kanuni ya" haki za binadamu kwa wote "inatumika kwa Wahaiti."

Hata hivyo Umoja wa Mataifa umendelea kusema kuhusu uhalali wake wa kisheria kwamba unalindwa na sheria za kidiplomasia na kwamba hawawezi kulipa walioathirika. Madai hayo yametupiliwa mbali na waathirika pamoja na familia za wahanga.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.