Pata taarifa kuu
SUDANI-ICC-BASHIR-SIASA-HAKI

ICC: Serikali ya Sudan yatoa msimamo wake kuhusu hatma ya Omar al-Bashir

Waziri wa Habari na msemaji wa serikali ya Sudan ameweka wazi msimamo wa serikali ya Khartoum kuhusu Omar al-Bashiri kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC.

Rais wa zamani wa Sudan Omar el-Bashir anaondoka ofisini kwa mwendesha mashtaka anayesimamia kesi za ufisadi huko Khartoum, Juni 16, 2019.
Rais wa zamani wa Sudan Omar el-Bashir anaondoka ofisini kwa mwendesha mashtaka anayesimamia kesi za ufisadi huko Khartoum, Juni 16, 2019. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumanne, mwakilishi mkuu wa Sudan alitangaza kwamba rais wa zamani wa Sudan Omar al-Bashir, katika siku za usoni, anaweza kuhamishiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai. Uamuzi ambao uliwashangaza wengi, kwa sababu Baraza Kuu tawala nchini Sudan lilikuwa limepinga uamuzi huo.

"Uamuzi huu unaungwa mkono kabisa na Baraza Kuu la Amani ambalo linajumuisha wajumbe wote wa Baraza Kuu tawala. Kwa hivyo hii ni pamoja na askari wa Baraza hili Kuu tawala. Wawili kati yao askari hao tayari wanashiriki katika mazungumzo haya ya amani yanayoendelea Juba, nchini Sudani Kusini. Tumekubaliana kuhusu kanuni ya wale wanaolengwa na waranti wa kukamatwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya JInai, ICC. Wako wanne. Mmoja wao ni Omar al-Bashir. Kuna Ahmed Haroun, Abdelrahim Mohammad Hussein na Ali Kosheib. Mengi tutayajadili baadaye. Tutazungumzia masuala hayo na wawakilishi wa ICC na makundi ya waasi ya Darfur wakati wa mazungumzo yanayoendelea huko Juba, " Waziri wa Habari wa Sudan Faisal Mohammed Saleh amesema.

Omar al-Bashir anatuhumiwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, pamoja na mauaji ya kimbari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.