Pata taarifa kuu
MALI-HRW-USALAMA

HRW yaitaka Mali kuchunguza kuhusu mauaji ya watu 450

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linaitaka serikali ya Mali, kuwachukulia hatua wanajihadi na wapiganaji wa kikabila ambao wamesababisha vifo vya watu 450 nchini humo mwaka uliopita.

Askari wa jeshi la Mali katika mazoezi ya kupambana na ugaidi. (Picha ya kumbukumbu).
Askari wa jeshi la Mali katika mazoezi ya kupambana na ugaidi. (Picha ya kumbukumbu). AFP PHOTO / PHILIPPE DESMAZES
Matangazo ya kibiashara

Human Rights Watch inasema kuwa, haya ndio mauaji mabaya dhidi ya raia ambayo yamewahi kushuhudiwa nchini humo tangu mwaka 2012.

Baada ya kuwahoji watu 147, Human Rights Watch inasema imebaina mauaji ya mamia ya watu hao na mamia kujeruhiwa, huku Mhubiri wa Kiislamu Amadou Koufa, akiongoza wapiganaji wa kikabila dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.

Tangu mwaka huo, Mali imekuwa ikipambana na ukosefu wa usalama, baada ya kuzuka kwa makundi ya kijihadi Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Magahribi.

Licha ya nchi hiyo kuwa na vikosi vya kigeni, ambao pia wapo nchini Burkina Faso na Niger katika vita dhidi ya makundi ya kijihadi.

Human Rights Watch inasema licha ya serikali ya Mali kuwafahamu wanaotekeleza mauaji haya, haiwachukulii hatua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.