Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-MAUAJI-USALAMA

Zaidi ya watu 100 wauawa ndani ya kipindi cha wiki mbili Burkina Faso

Nchi ya Burkina Faso inaendelea kukumbwa na jinamizi la mauaji kufuatia mashambulizi mbalimbali ya makundi watu wenye silaha. Raia ndio wanaendelea kulengwa zaidi katika mashambulizi hayo.

Ni katika kijiji cha Lamdamol, katika Wilaya ya Bani, ambapo zaidi ya watu 20 waliuawa katika shambulio la wanamgambo wa Kiislamu.
Ni katika kijiji cha Lamdamol, katika Wilaya ya Bani, ambapo zaidi ya watu 20 waliuawa katika shambulio la wanamgambo wa Kiislamu. RFI
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya raia ishirini waliuawa usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili Februari 2, 2020 katika "shambulio la lilotekelezza na wanamgambo wa Kiislamu" huko Lamdamol, kijiji cha kaskazini mwa Burkina Faso, kwa mujibu wa chanzo cha usalama.

"Watu wasiojulikana waliojihami kwa silaha za kivita walishambulia kijiji cha Lamdamol usiku wa Jumamosi kuakia Jumapili, na kuua zaidi ya raia 20," chanzo cha usalama kimeliambia shirika la Habari la AFP.

"Washambuliaji wenye silaha za kivita waliokuwa kwenye pikipiki waliuaa wakazi wengi wa eneo hilo" linalopatikana katika Tarafa ya Bani, kilomita 40 kutoka Gorgadji, katika mkoa wa Séno.

Kulingana na mfanyakazi wa afya huko Dori, aliyehojiwa na shirika la Habari la AFP, "muuguzi mkuu wa kituo cha afya cha eneo hilo, ambaye aliyekuwa akirejea kazini katika kijiji cha Lamdamol, aliuawa katika shambulio hilo".

"Wakaazi wameingiliwa na hofu katika kijiji hicho na maeneo jirani. Watu wamekimbilia maeneo wanaoamini kwamba ni salama, hata wakaazi wa eneo la Gorgadji wamehama makaazi yao, "mgfanya kazi huyo wa afya ameongeza.

Chanzo kingine cha usalama, kilichohojiwa na shirika la Habari la AFP, kimethibitisha shambulio hilo, na kubaini kwamba ni shambulio la "kulipiza kisasi dhidi ya wakaazi ambao siku chache zilizopita, walitakiwa kuondoka katika maeneo hayo".

Januari 25i, raia 39 waliuawa katika shambulio la wanamgambo wa Kiislamu, katika kijiji cha Silgadji, mji unaopatikana katika Wilaya ya Tongomayel, katika Mkoa wa Soum.

Burkina Faso, inayopakana na Mali na Niger, inakabiliwa na mashambulio ya wanamgambo wa Kiislamu ambayo yameua karibu watu 800 tangu mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.