Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Watu wengi wauawa katika makabiliano Bria, Jamhuri ya Afrika ya Kati

Serikali ya Jamhri Afrika ya Kati imeendelea kusalia kimya kuhusu idadi ya watu waliouawa katika makabiliano ya kikabila yaliyotokea Jumamosi wiki iliyopita katika mji wa Bria, Mashariki lmwa nchi hiyo.

Makao lmakuu ya polisi ya Bria, Jamhuri ya Afrika ay Kati, Machi 11, 2015.
Makao lmakuu ya polisi ya Bria, Jamhuri ya Afrika ay Kati, Machi 11, 2015. RFI/Pierre Pinto
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano hayo yaliyotokea kati ya makundi mawili ya waasi wa zamani wa Seleka yaliendelea hadi Jumapili.

Mapigano ya mwishoni mwa wiki iliyopita huko Bria yaligharimu maisha ya watu wengi. Watu 35 waliuawa kwa mujibu wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Idadi ambayo inaweza kufikia hadi 50, kwa mujibu wa meya wa mji huo.

Mji wa Bria ulikuwa hauingiliki siku ya Jumapili kutokana na machafuko hayo na mazishi yalifanyika haraka na na hivyo kusababisha idadi sahihi ya watu waliouawa katika makabiliano hayo kutojulikana.

Watu 11, 000 walitoroka makaazi yao kufuatia makabiliano hayo, kwa lujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura (OCHA).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.