Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-MAUAJI-USALAMA

Burkina Faso: Raia wengi waua katika shambulio Silgadji

Watu wengi wameangamia katika shambiulio jipya dhidi ya raia katika kijiji cha Silgadji, mkoani Soum, nchini Burkina Faso. Shambulio hilo lilitokea Jumamosi, lakini taarifa kuhusu shambulio na idadi ya watu waliouawa ilitolewa mapema wiki hii na mamlaka nchini Bukina Faso.

Silgadji, katika mkoa wa Soum
Silgadji, katika mkoa wa Soum RFI
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliouawa katika shambulio hilo inatofautiana kulingana na vyanzo mbalimbali: kati ya watu 10 hadi 50 waliuawa kwenye soko la kijiji Silgadji, nchini Burkina Faso.

Watu wenye silaha walifanya shambulio dhidi ya raia kwenye soko soko la kijiji Silgadji, kulingana na vyanzo vyetu.

"Washambuliaji waliwakusanya raia sehemu moja. Halafu wakatenganisha wanawake na wanaume. Wanaume wote waliuawa na wanawake wakaachiliwa" , chanzo cha serikali kimebaini.

Kwa mujibu wa shahidi mmoja, aliyenukuliwa na ofisa wa serikali katika eneo hilo, washambuliaji walikagua vitambulisho vya wanaume hao kabla ya kuwauwa.

Kulingana na chanzo chetu cha usalama, washambuliaji waliharibu mitambo inayotoa huduma ya mawasiliano kwa simu, ili kuzuia mawasiliano yoyote na maeneo mengine.

Ni vigumu kutoa idadi ya watu waliouawa katika shambulio hili. Kati ya watu 10 na 50 waliuawa, kulingana na vyanzo kadhaa. Lakini idadi hii inaweza kuzidi, kwa sababu kuna watu waliotoweka kulingana na chanzo cha usalama ambacho kilikutana na watu walionusurika shambulio hilo.

Kulingana na chanzo cha serikali, washambuliaji haowalitega vilipuzi kwenye barabara zinazoingia katika kijiji hicho. Ni vigumu kwa vikosi vya usalama kuingia na magari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.