Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Nchi jirani na Libya waunga mkono makubaliano ya kusitisha vita

Mawaziri wa Mambo ya nje wa nchi zinazopakana na Libya wamekutana leo Alhamisi nchini Algiers kujaribu kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya vikosi vya Marchal Khalifa Haftar, na vile vya serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na Fayez al Sarraj.

Mawari kutoka chi za Misri, Tunisia, Sudan, Chad, Mali na Niger katika mkutano Algiers kuhusu kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano Libya;
Mawari kutoka chi za Misri, Tunisia, Sudan, Chad, Mali na Niger katika mkutano Algiers kuhusu kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano Libya; REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu, ambao umezileta pamoja, Misri, Tunisia, Sudan, Chad, Mali na Niger , ni moja ya jitihada za kimataifa baada ya mkutano uliyofanyika Jumapili iliyopita jijini Berlin, nchini Ujerumani.

"Majirani wa Libya wanabeba jukumu la kuwezesha kupatikana kwa suluhisho la kisiasa," amesema waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Sabri Boukadoum kabla ya mkutano kufunguliwa.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas, amefanya ziara jijini Algiers.

Libya imeendelea kukabiliwa na ukosefu wa usalama na amani baada ya utawala wa Muammar Gaddafi, kuanguka mwishoni mwa mwaka wa 2011. Jumuiya ya kimataifa, hasa nchi zinazopaka na Libya zinaendelea kuwa na wasiwasi baada ya kuongezeka kwa mgogoro unaoshuhudiwa tangu vikosi vya Marshal Haftar kuzinduwa mashambulizi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli, katika msimu wa baridi mwaka uliopita.

"Ukanda mzima wa Sahel anaathirika kutokana na mgogoro huo wa Libya. Kutapakaa kwa silaha katika ukanda huo kumewezesha ugaidi kuzidi kusambaa," Waziri wa Mambo ya nje wa Chad, Mahamet Zene Cherif, amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.